
Umeshawahi kujiuliza kwanini mpaka leo kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kina uchache wa Magwiji katika mixing & mastering??? Majina kama Laizer, Mixing killer, Chizan Brain n.k yanatajwa kwa kujirudia kwenye nyimbo za wasanii wengi kwasasababu ni wao tu ndo walioamua kujiongeza kwa kupata knowledge ya ukamilishaji wa project za Audio.Naomba nikukaribishe kwenye ulimwengu wa Chizan Brain, kijana mzaliwa wa Ifakara, Hospitali ya Mtakatifu Francisi, akakulia Tanzania, mpaka alipohamia Kenya kwa Baba yake kumalizia elimu yake sekondari na chuo. Na ndiko aliko anzia safari yake ya muziki kwani Mzee wake pia ni mwanamuziki hodari katika kupiga vyombo takribani vyote, gitaa likiwa ndio chaguo lake la muda mwingi. Akiwa moja wapo wa waanzilishi wa Ukoo flani, akapita studio kadhaa Kenya na muda ulipo fika akahamishia makazi yake nchini Tanzania na kuendelea kukinukisha kwenye tansia ya Muziki wa kizazi kipya. Mezani, Chizan amefunguka kwa kina kuhusu safari yake nzima ya mziki. Karibu ujumuike nasi mezani kumfahamu mkali huyu!!