
ย Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao waย Facebookย huenda umewahi kukutana na chapisho linalohusu fursa ya mikopo kutoka kwenye taasisi ya mfanyabiashara bilionea nchini Tanzania Mohamed Dewji Foundation
Sehemu ya chapisho hilo lianasomeka โ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ kwa maelekezo ya kupata vigezo na masharti njoo hwatspp kwa no๐๐ฟ 0748923136โ.
Chapisho hilo pamoja na kuhamasisha watu kuomba mikopo wametaja kigezo cha kutoa kwanza kiasi cha hisa ya mkopo unaotaka kupewa kabla ya kupata mkopo wenyewe.
Ufafanuzi zaidi wa taarifa hiyo unaonesha kama unahitaji kukopa Sh100,000 basi utalazimika kutoa kwanza hisa ya Sh22,000 ndipo upewe mkopo huo.
Taarifa hiyo imesambaa katika mtandao wa Facebook kupitia akaunti zenye majina tofauti tofauti toka mwakaย 2022ย huku ikiwa imeambatanishwa na ย video fupiย inayomnukuu Mohamed Dewji kuwa anatoa mikopo.
Hata hivyo, Habari hiyo haina ukweli wowote kwa kuwa ni habari za uzushi zinazotumiwa na matapeli kuwalaghai wananchi na kujipatia vipato kwa njia zisizo halali.ย
Nukta Fakti imefanya utafiti ili kubaini ukweli wa akaunti hizo za mtandao wa Facebook na kugundua kuwa akaunti hizo hazina uhusiano wowote na Mohamed Dewji mwenyewe au taasisi yake ya Mohamed Dewji Foundation.
Akaunti sahihi ya Facebook ya mfanyabiashara huyo maarufu nchini niย Mohammed Dewjiย huku ile ya taasisi yake niย Mo Dewji Foundationย na sioย Mikopo Tanzaniaย kama inavyojitambulisha akaunti hiyo inayodai kutoa mikopo.
Mohamed Dewji hatoi mikopo
Utafiti zaidi uliofanywa na Nukta Fakti umebaini kuwa, siย Mohamed Dewjiย mwenyewe walaย taasisi yakeย ambayo inajihusisha na utoaji wa mikopo kwa namna yoyote ile.
Kupitia mtandao waย Linkedin Mohamed Dewjiย amewahi kutoa taarifa kwa umma akifafanua kuwa taasisi yake inajihusisha zaidi kutoa misaada ya kielimu kwa kufadhili masomo, upatikanaji wa maji pamoja na kutatua changamoto katika sekta ya afya.