Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anatuelimisha namna ya matumizi ya neno "KUKANIA"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anatuelimisha namna ya matumizi ya neno "KUKANIA"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anatuelimisha namna ya matumizi ya neno "KUKANIA"
Miaka 80 iliyopita baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, mataifa 50 yalikutana huko San Francisco hapa nchini Marekani na kupitisha Chata iliyoanzisha Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa malengo ni kuzuia vita na kujenga uhusiano mwema baina ya mataifa. Mathalani kuepusha nchi moja kuvamia nchi nyingine na kulinda haki za binadamu. Leo hii Chata hiyo imeendelea kusiginwa na kilichoibua mjadala zaidi ni tukio la Januari 3 la Vikosi Maalum vya Marekani kuingia Venezuela na kumtwaa Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro pamoja na mkewe kwa madai ya kwamba wanatakiwa wajibu tuhuma nchini MArekani za uhalifu mkubwa ikiwemo usafirishaji wa dawa za kulevya. Je Chata hiyo inasema nini? Assumpta Massoi na Rashid Malekela wanapitia baadhi ya vifungu pamoja na yaliyojiri baada ya hatua ya Marekani.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Chata iliyoanzisha Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kukutanisha mataifa 50 San Francisco hapa Marekani na kupitisha Chata hiyo, ikilengaa kuzuia vita na kujenga uhusiano mwema baina ya mataifa.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA), nchini Burundi, linaongeza juhudi zake kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wanaokimbia mapigano yanayoendelea mashariki taifa hilo la Maziwa Makuu ili kulinda afya, usalama na utu wao na wa jamii zinazowapokea. Sheilah Jepng’etich na taarifa zaidi
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo katika kikao cha dharura baada ya operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela tarehe 3 Januari mwaka huu, hatua iliyozua hofu ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu nchini humo na katika eneo zima. Leah Mushi anatufahamisha zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia hali nchini Venezuela operesheni ya kijeshi ya Marekani, afya ya uzazi Tana River nchini Kenya, na wanawake wakimbizi wa DR Congo wanaopitia ukatili wa kijinsia wakikimbia machafuko.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Huko nchini Kenya katika kaunti ya Tana River, hali mbaya ya hewa na migogoro imesababisha takriban watu 140,000 kuyahama makazi yao. Upatikanaji wa huduma za afya nao umekuwa mgumu na kuongeza magumu hususani kwa wanawake na watoto. Katika kukabiliana na hali hiyo Wizara ya Afya nchini humo inashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO katika kutoa huduma za afya kipaumbele kikielekezwa kwenye masuala ya uzazi salama. Rashidi Malekela na taaria zaidi
Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFP limechukua hatua kukabiliana na changamoto ya mimba za utotoni zinazochochewa na vikwazo vya kijamii na utamaduni pamoja na upungufu wa huduma za afya ya uzazi na kijinsia zinazofaa kwa vijana. Msichana mmoja anasimulia masaibu aliyopita katika taarifa hii ya Sheilah Jepngetich.
Nchini Zambia, mafunzo ya mapishi yanayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto, UNICEF, kwa wanawake yamefanikiwa kubadilisha namna familia zinavyowalisha watoto wao, kwa kutumia vyakula ambavyo tayari vinapatikana katika mazingira yao. Taarifa zaidi na Leah Mushi.
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi kutoka DR Congo wanaokimbilia Burundi, lishe bora kwa watot nchini Zambia, na afya ya uzazi na msaada wa UNFPA kwa wasichana vijana nchini Kenya.
Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Kilio cha wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC cha kupatiwa msaada ukiwemo wa chakula kimeitikiwa na Japani, moja ya mdau wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ambapo shirika hilo limepatiwa dola laki sita na elfu ishirini na tano, kama anavyosimulia Assumpta Massoi.
Kutana na Maseka ambaye ni miongoni mwa makumi ya maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waliovuka mpaka na kuingia nchi Jirani ya Burundi baada ya ghasia kulazimisha familia yake kukimbia mashariki mwa DRC. Flora Nducha na taarifa zaidi
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema ukosefu wa chakula utaendelea kuwa katika viwango vya kutisha katika mwaka ujao wa 2026, huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na njaa kali duniani. Leah Mushi na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WFP ya uhakika wa chakula mwaka 2026 duniani, wakimbizi kutoka DRC, waliovuka mpaka na kuingia Burundi, na kilimo cha umwagiliaji kwa jamii za Hirshabelle nchini Somalia.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Jamii za wakulima katika mkoa wa middle Shabelle, Somalia, zimeathiriwa vibaya na ukame na mafuriko yanayodhoofisha kilimo na uhakika wa chakula. Ili kukabiliana na hili, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Somalia kwa ufadhili wa Serikali ya Uswisi imetekeleza mradi wa BRiMS unaolenga kuimarisha mnepo kwa wakulima kupitia ukarabati wa miundombinu ya vijijini, urejeshaji wa mifumo ya umwagiliaji, na kuijengea jamii uwezo. Sheilah Jepng’etich na taarifa zaidi.
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Anold Kayanda anakuletea Jarida Maalum linalomulika Maoni ya washirika wetu mbalimbali wa Televisheni na Radio kutoka Afrika Mashariki.
Wanazungumzia umuhimu wa ushirika na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa
Yale waliyofaidika nayo katika ushirika huu na nini kiboreke mwakani
Mapendekezo yao kwa mwaka ujao wa 2026
Na salamu zao za mwaka mpya 2026
Huko kaskazini mashariki mwa Somalia, eneo la Laascaanood linaendelea kushuhudia maboresho ya huduma muhimu za afya baada ya miaka miwili ya kuvurugika kwa huduma hizo kutokana na mizozo, maboresho haya yanaleta huduma za afya karibu zaidi na akina mama na watoto shukran kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na washirika wake. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
(Taarifa ya Leah)
Kwa mujibu wa UNICEF nchini Somalia, mamilioni ya watoto wanakua katika kivuli au mazingira ya ukimya na dharura zilizosahaulika, takribani watoto milioni 1.8 wanahitaji matibabu ya utapiamlo mwaka huu wa 2025. Kila mwaka watoto wapatao 75,000 walio chini ya umri wa miaka mitano hufariki dunia kutokana na magonjwa yanayozuilika na yanayoweza kutibiwa.
Miaka miwili ya migogoro imesababisha kusambaratika kwa huduma muhimu huko Laascaanood. Kurejea kwa hali ya utulivu kumeanza kushuhudia urejeshwaji wa taratibu wa huduma hizi muhimu zinazookoa maisha. UNICEF, kwa msaada wa KSRelief na Saudi Esports Federation, inachangia kwenye kutoa huduma jumuishi za afya ya msingi, huku huduma hizo zote zikitolewa chini ya paa moja.
Mpaka sasa maelfu ya watu wamefikiwa huku ukisaidia vituo 13 vya afya kama anavyoeleza Dayid Said Ismail Afisa Lishe
(Sauti ya Dayid Said Ismail – Evarist)
“Mradi huu unasaidia vituo 13 vya afya na unahudumia zaidi ya watu 150,000. Huduma zake zinajumuisha chanjo za watoto, matibabu ya magonjwa kama nimonia na kuhara, pamoja na huduma za magonjwa mengine ya kawaida ya utotoni.”
Katika huduma za matibabu tumsikilize Saida Ali Elmi ambaye ni mhudumu wa Afya
(Sauti ya Saida Ali Elmi- Sheilah)
“Kama mnavyoona, akina mama wengi wamekuwa kwenye foleni tangu saa moja asubuhi na sasa ni saa 5:30 asubuhi. Kwa hiyo wapo hapa kwa ajili ya chanjo za kinga, ikiwemo chanjo za kifua kikuu, surua, polio, pepopunda, kifaduro, pamoja na chanjo mpya iitwayo PCV ya nimonia.”
Juhudi hizi zinazofanywa na mashirika haya, tayari zimeanza kuleta matumaini mapya kwa Ayan Hassan Abdi mama mzazi wa Maryam “Nimemleta Maryam kwa sababu alikuwa na homa. Amepatiwa matibabu na pia chanjo. Alifanyiwa vipimo vya homa na kuharisha, na akatibiwa vizuri, Masha’Allah.”
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
-Katika ujumbe wake wa mwaka mpya 2026 Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres ameitaka dunia kushikamana kwa ajili ya amani, maendeleo, na usalama badala ya kuongeza mateso
-Huko Somalia kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wakaazi wa Laascanood waboreshewa huduma za afya baada ya kuvurugika kwa miaka miwili
-Na Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO amesema mwaka 2025 ulighubikwa na changamoto lukuki za afya ya umma duniani ikiwemo ukata wa ufadhili, lakini kuna matumaini hasa katika suala la utipwatipwa