Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Business
Society & Culture
History
Sports
Technology
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts122/v4/94/24/4c/94244c26-3c27-edd3-2e5e-012b22a7bb93/mza_1137301887147468075.jpg/600x600bb.jpg
Jukwaa la Michezo
RFI Kiswahili
24 episodes
4 days ago

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.

Show more...
Sports
RSS
All content for Jukwaa la Michezo is the property of RFI Kiswahili and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.

Show more...
Sports
Episodes (20/24)
Jukwaa la Michezo
Uchambuzi wa Mada: Je, AFCON 2025 inatoa msisimko kama mashindano yaliyopita?
Leo tunajadili kwa undani kauli ya kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos kuwa michuano ya mwaka huu haina mvuto na msisimko kama Afcon zilizopita. Uchambuzi wa mechi za jana na leo kwenye hatua ya 16 bora - Tanzania vs Morocco, Afrika Kusini vs Cameroon, DRC vs Algeria. Hatua ya serikali ya Gabon kuvunjilia mbali timu ya Gabon huku marais wa Msumbiji na Benin wakitoa ahadi za pesa kwa timu zao. Morocco kuandaa michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu 2029 nayo Ethiopia ikiwania kuandaa Afcon ya 2028.
Show more...
1 week ago
24 minutes 34 seconds

Jukwaa la Michezo
AFCON 2025: Mtazamo wa hatua ya mtoano, timu 16 zitawania tiketi ya fainali
Leo tumeangazia kwa undani matokeo na matukio ya hatua ya makundi iliyokamilika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea Morocco, uchambuzi wa hatua ya 16 bora - nani atafuzu robo fainali?, tathmini ya hatua ya serikali ya Gabon kuvunja kabisa timu ya taifa ya Gabon, ahadi za pesa kutoka kwa marais kadhaa Afrika kwa timu zao kuelekea robo fainali, usajili wa Rayon Sport, kwa nini Maresca aliondoka Chelsea?, dereva wa Anthony Joshua afunguliwa mashtaka baada ya ajali Nigeria.
Show more...
1 week ago
23 minutes 48 seconds

Jukwaa la Michezo
AFCON 2025: Morocco dhidi ya Comoros kufungua mashindano leo usiku
Leo tunaangazia pakubwa kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025; tunachambua mechi ya ufunguzi kati ya Morocco na Comoros, mjadala kuhusu mageuzi katika michuano hii, namna timu zilivyotua nchini Morocco kwa kuvalia mavazi ya kitamaduni, Morocco wapo kwenye shinikizo ya kunyakua ubingwa kwa kuwa mwenyeji lakini pia ubashiri wa mechi ya ufunguzi na atakayebeba taji la mwaka huu.
Show more...
3 weeks ago
24 minutes

Jukwaa la Michezo
AFCON 2025: Mashindano kufanyika kila baada ya miaka minne baada ya 2028
Usiku mmoja kabla ya kuanza kwa michuano ya Afcon 2025 tunakufahamisha mambo yote unayostahili kujua pamoja na mabadiliko ya michuano hii kuendelea mbele, michezo ya chipukizi ya Afrika yatamatika Angola, Rayon Sports na Simba zapata makocha wapya, mkenya David Munyua aweka historia katika mchezo wa darts duniani, Anthony Joshua amlaza Jake Paul kupitia knockout, droo ya nusu fainali ya kombe la Carabao.
Show more...
3 weeks ago
23 minutes 56 seconds

Jukwaa la Michezo
CAF: Wachezaji gani wameitwa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2025?
Leo tunachambua vikosi vilivyotajwa na mataifa kuelekea Kombe La Mataifa ya Afrika nchini Morocco, Ligi ya Afrika ya basketboli ya kina dada imeingia hatua ya nusu fainali, michezo ya chipukizi ya Afrika inayoendelea Angola, mabadiliko katika mashindano ya Tour du Rwanda, mechi za kufuzu mashindano ya shule za upili ya CAF, Ben Sulayem achaguliwa kuendelea kuongoza shirikisho la kimataifa la mchezo wa magari, sakata la MoSalah klabuni Liverpool na ziara ya Messi huko India yazua rabsha.
Show more...
4 weeks ago
23 minutes 53 seconds

Jukwaa la Michezo
Droo ya Kombe la Dunia 2026: Fahamu makundi ya michuano hii ya mwakani
Tuliyukuandalia leo ni pamoja na timu za Afrika zimepangwa kwenye makundi gani katika Kombe la Dunia la mwaka ujao, nani ataibuka na taji la Formula 1 kesho, Kenya kuandaa mashindano ya dunia ya Taekwondo, michuano ya kufuzu mashindano ya shule za upili barani Afrika, kuanza kwa Ligi ya Afrika ya basketboli ya wanawake, wachezaji wa soka Afrika waanzisha kampeni dhidi ya polio, Onana na Aboubakar watemwa kikosini Cameroon huku nahodha wa Nigeria Troost Ekong akistaafu soka la kimataifa.
Show more...
1 month ago
23 minutes 55 seconds

Jukwaa la Michezo
Washikadau wa Fencing Afrika Mashariki waziomba serikali za Afrika kusaidia ukuaji wa mchezo
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kilio cha washikadau wa mchezo wa fencing Afrika Mashariki kwa serikali za Afrika kusaidia kukuza mchezo, mashindano ya Tong Il Moo Do yarejea tena nchini Kenya baada ya marufuku ya mwaka mmoja, uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Afrika, Sudan Kusini yaanza vyema michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la Basketboli 2027, mfaransa Sebastian Ogier akaribia kushinda taji la dunia la tisa, uchambuzi wa mechi za ligi ya mabingwa Ulaya.
Show more...
1 month ago
23 minutes 59 seconds

Jukwaa la Michezo
CAF: Achraf Hakimi ashinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2025
Leo tumezingatia tuzo za CAF 2025, AS FAR yaibuka washindi wa kombe la Ligi ya Afrika ya kina dada, kuanza kwa michuano ya klabu bingwa Afrika kwa wanaume huku AS FAR ikinyakua taji la kina dada, matokeo ya mechi za kufuzu AFCON U17 ukanda wa Cecafa, Curacao yakuwa taifa dogo zaidi kuwahi kufuzu Kombe la Dunia huku Marekani ikizindua mfumo maalum wa kutoa visa kwa wanunuaji tiketi.
Show more...
1 month ago
23 minutes 54 seconds

Jukwaa la Michezo
KPA (Kenya), APR na REG za Rwanda zafuzu Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika kwa kina dada
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kuanza kwa michuano ya raga ya Afrika kwa kina dada wachezaji saba kila upande, michuano ya kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika kwa kina dada, ligi ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 - Gattuso asema Afrika inafaa kupewa nafasi chache, uchaguzi wa Kamati kuu ya Olimpiki nchini DRC, bingwa wa dunia Beatrice Chebet apokea tuzo ya kitaaluma.
Show more...
1 month ago
23 minutes 53 seconds

Jukwaa la Michezo
Miguel Gamondi kuiongoza Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2025 Morocco
Tuliyokuandalia ni pamoja na kocha Gamondi kuteuliwa kuwa kaimu kocha wa Tanzania, Kipchoge akutana na Obama, Tume Huru ya Uchaguzi ya Kamati ya Olimpiki ya Kongo yachapisha orodha ya mwisho ya wagombea, kukosekana kwa Beatrice Chebet na Faith Kipyegon kwenye tuzo za mwanariadha bora wa mwaka, makundi ya michuano ya afrika ya raga kwa kina dada na mechi za kufuzu Ligi ya Afrika ya Basketboli, droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika, uchambuzi wa matokeo ya ligi ya mabingwa Ulaya
Show more...
2 months ago
23 minutes 57 seconds

Jukwaa la Michezo
Kenya na Tanzania zafuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON2026)
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Sudan kusherehekea kambi ya kwanza kabisa ya ndondi ya wanawake nchini humo, Nairobi itakuwa mwenyeji wa michuano ya kufuzu ligi ya afrika ya basketboli mwezi huu, Kinshasa itaandaa michuano ya kitaifa ya ndondi ya chipukizi, Tanzania na Kenya zimefuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada mwaka 2026, Ethiopia itaandaa michuano ya kufuzu AFCON U17, ratiba ya mechi za mchujo kufuzu Kombe la Dunia, Paris Masters, Pogba apata jeraha jipya.
Show more...
2 months ago
23 minutes 44 seconds

Jukwaa la Michezo
WAFCON: Michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika ipo raundi ya mwisho
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na waamuzi watatu nchini Rwanda kusimamishwa kwa muda, Kongamano la nne la Kibiashara la Soka lakamilika nchini Kenya, awamu ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, tuzo za CAF mwaka huu, mechi za kufuzu hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika, mkenya Ruth Chepngetich apigwa marufuku ya miaka mitatu, bingwa wa dunia wa MotoGP Marquez kukosa msimu mzima uliosalia na nusu fainali ya tenisi Vienna Open
Show more...
2 months ago
23 minutes 51 seconds

Jukwaa la Michezo
FIFA: Ni mataifa gani ya Afrika ambayo tayari yamefuzu Kombe La Dunia mwaka 2026
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na tathmini ya timu za Afrika ambazo zimefuzu Kombe la Dunia 2026 na ni nani ambao wana nafasi ya kufuzu kuelekea raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu, FIFA yateua wajumbe kutoka CECAFA, Herita Ilunga ndiye mkurugenzi mpya wa FECOFA nchini DRC, kocha wa zamani wa Yanga Nassredine Nabi waachana na Kaizer Chiefs, nyota tajika wa tenisi duniani wabwagwa kwenye mashindano ya Wuhan Open, Rovapera kustaafu mchezo wa kuendesha magari
Show more...
3 months ago
24 minutes 3 seconds

Jukwaa la Michezo
Mashindano ya boti za umeme zinafanyika Afrika kwa mara ya kwanza Lagos, Nigeria
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Rwanda kuwa taifa la kwanza Afrika kudhamini vilabu vya basketboli Ulaya, nini kinachoendelea klabuni Simba washikadau wanaendelea kuondoka, TP Mazembe yajiondoa katika Chama cha Vilabu vya Soka vya Kongo, Afrika inaandaa kwa mara ya kwanza mashindano ya boti za umeme nchini Nigeria, mwanawe Zidane aitwa kikosini Algeria, FIFA yazindua mpira utakaotumika mwaka ujao kwenye Kombe la Dunia, Hamilton akabiliwa na uchunguzi kuelekea mkondo wa Singapore.
Show more...
3 months ago
23 minutes 57 seconds

Jukwaa la Michezo
Waafrika wa kutazama kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Tokyo, Japan
Tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa mashindano ya riadha ya dunia, michuano ya Cecafa inayoendelea kwa kina dada na wanaume, Simba Day na Yanga Day huko Tanzania, michuano ya basketboli ya Afrika ya wavulana wasiozidi miaka 16, kinachotarajiwa baada ya rabsha katika mechi ya DRC na Senegal
Show more...
4 months ago
23 minutes 51 seconds

Jukwaa la Michezo
Morocco ni timu ya kwanza ya Afrika kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya mechi za kufuzu kombe la dunia la mwaka ujao, mechi za kufuzu mashindano ya vilabu bingwa kwa kina dada ukanda wa CECAFA, mashindano ya CECAFA Kagame Cup, wanariadha watatu wa Uganda kukosa Riadha za Dunia mwezi huu nchini Japan, rais wa Marekani Donald Trump kuhudhuria fainali ya wanaume ya US Open, Luis Suarez apewa adhabu ya mechi sita baada ya kumtemea mate mwanachama wa benchi la ufundi ya klabu ya Seattle Sounders.
Show more...
4 months ago
24 minutes 16 seconds

Jukwaa la Michezo
CHAN 2024: Nani atashinda kati ya Morocco na Madagascar ?
Morocco na Madagascar zinachuana katika fainali ya mchezo wa CHAN 2024. Hii ni michuano inayowashirikisha wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani. Fainali hii inachezwa kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kasarani, Agosti 30 2025. Wanamichezo wetu Jason Sagini na Paul Nzioki, wanachambua kutoka uwanjani.
Show more...
4 months ago
20 minutes 58 seconds

Jukwaa la Michezo
CHAN 2024: Wenyeji Kenya, Uganda na Tanzania watupwa nje ya mashindano
Leo tumekuandalia mengi ikiwemo kubanduliwa kwa Kenya na Tanzania kwenye michuano ya CHAN katika hatua ya robo fainali, michuano ya basketboli ya Afrika ya wanaume imeingia hatua ya nusu fainali, shirikisho la soka nchini Sudan Kusini limetangaza tarehe mpya ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya wanawake, Wan Bissaka ajumuishwa katika kikosi cha soka cha DRC, Mohammed Salah ashinda tuzo la mchezaji bora wa wachezaji kwa mara nyingine.
Show more...
4 months ago
23 minutes 52 seconds

Jukwaa la Michezo
CHAN 2024: Kenya, DRC, Morocco zafukuzia ushindi mechi za mwisho za makundi
Leo tumekuandalia uchambuzi wa timu ambazo zimefuzu, gani zimeondolewa na nani wanaweza kufuzu hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Chan, michuano ya baskeboli ya wanaume ya Afrika, viongozi wa mashabiki Sudan Kusini waandaa mechi ya kirafiki kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, rais wa AS Kigali aahidi kuongeza tuzo za ligi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa shirikisho, Alcaraz afuzu robo fainali michuano ya Cincinnati Open.
Show more...
4 months ago
21 minutes 13 seconds

Jukwaa la Michezo
CHAN 2024: Kenya yafukuzia ushindi dhidi ya Morocco, Tanzania ikihitaji sare tu
Leo tumekuandalia uchambuzi, matokeo na matukio ya raundi ya pili ya hatua ya makundi ya michuano ya CHAN pamoja na mechi za leo usiku na kesho mchana, droo ya michuano ya awali ya kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa barani Afrika, uhamisho wa wachezaji Afrika Mashariki huku Kinshasa ikichaguliwa kuandaa mkutano mkuu wa CAF mwezi Oktoba, Thomas Partey kujiunga na Villareal licha ya kesi za ubakaji, 
Show more...
5 months ago
23 minutes 52 seconds

Jukwaa la Michezo

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.