Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Business
Society & Culture
History
Sports
Technology
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts221/v4/da/ea/21/daea2180-3e60-bbe4-7acf-9eefafd9acf8/mza_6934734439202477976.jpg/600x600bb.jpg
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
RFI Kiswahili
24 episodes
1 day ago

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Show more...
Science
RSS
All content for Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho is the property of RFI Kiswahili and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Show more...
Science
Episodes (20/24)
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Awamu ya pili: Matukio muhimu ya mazingira na tabianchi mwaka wa 2025
Katika awamu ya kwanza tuliangazia miaka kumi ya mkataba wa tabianchi wa Paris na ahadi mpya za kitaifa NDCs. Awamu  ya pili na mwisho tunaendelea kuangazia mkutano wa tabianchi COP30 uliofanyika jijini Belem, Brazil, pamoja na mkutano wa saba wa kimataifa wa mazingira UNEA-7 uliofanyika jijini Nairobi kati ya Disemba 8 na 12 ùwaka wa 2025.
Show more...
4 days ago
9 minutes 57 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Awamu ya kwanza:Matukio muhimu ya mazingira na tabianchi 2025
1 week ago
9 minutes 53 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Wanaharakati wataka uhifadhi wa msitu wa mvua wa Kongo kupewa kipaumbele
Misitu ya mvua barani Afrika kimsingi imejikita katika Bonde kubwa la Kongo, msitu wa pili kwa ukubwa duniani wa kitropiki, unaohifadhi wanyamapori wa kipekee kama sokwe, na tembo wa msituni, pamoja na maeneo mengine muhimu kama vile Misitu ya Guinea ya Afrika Magharibi, misitu ya Afromontane Mashariki, na misitu ya pwani kutoka Kenya hadi Msumbiji yenye misitu ya kipekee ya kisiwa cha Madagaska.
Show more...
2 weeks ago
9 minutes 8 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Lugha ya kiswahili katika kuimarisha uelewa, uhamasishaji na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
Wakati viongozi wa dunia, wanasayansi na watunga sera wanapokutana katika miji mikuu ya Dunia kujenga hoja kuhusu hatima ya sayari kupitia mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa,  Wataalamu wa lugha,,  walimu pamoja na  wanafunzi waaendeleza  mijadala. Kaulimbiu ukiwa ni namna lugha adimu ya kiswahili inavyotumika katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Show more...
3 weeks ago
10 minutes 3 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Kituo cha jambo Redio nchini DRC chapokea tuzo kwenye COP30
Nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kituo cha Jambo redio, kimejitwika jukumu la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya mazingira na tabianchi, lakini muhimu sana ni haki zao. Katika mkutano wa tabianchi uliotamatika jijini Belem nchini Brazil, kituo cha Jambo Redio kilipokea tuzo kutoka kwa shirikika linalotetea haki za wanawake Women Engage for a Common Future, WECF. Kituo hiki, kimekuwa kikitoa habari kwa jamii ambazo wakati mwingine hazina uwezo wa kupata habari.
Show more...
3 weeks ago
10 minutes

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
COP30 uliotamatika jijini Belem, Brazil,, suala la ufadhili wa tabianchi, nishati safi ni miongoni mwa ajenda
  Miongoni mwa mambo yalioamuliwa ni kuhamasisha kiasi cha fedha trilioni 1.3 kila mwaka kufikia 2035 wa ajili ya hatua za tabianchi, kuimarisha fedha uhimilivu mara tatu kufikia 2035. Msikilizaji, suala la kuharakisha ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inasalia kuwa kipaumbele  cha dharura hasa kwa nchi zinazoendelea ambazo zina athirika pakubwa na janga hilo.
Show more...
1 month ago
9 minutes 59 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Shirika la Weather Mtaani labuni teknolojia ya kuepuka majanga ya hali ya hewa Kibera
Mvua huja kwa sauti ya baraka lakini katika kitongoji, sauti hiyo hubeba hofu. Maji yanapoteremka kutoka angani, katika sekunde chache, barabara hugeuka mito. Vyumba vya kulala vinageuka mabwawa. Katika kitongoji cha Kibera jijini Nairobi nchini Kenya, hali hiyo ya hofu imebadilishwa kupitia kundi la vijana linalojiita Weather Mtaani.
Show more...
1 month ago
9 minutes 57 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP30 jijini Belem, Brazil
Mkutano huu unakwenda kufanyika wakati ripoti mpya ya shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP, ikionesha kuwa bado dunia iko nyuma katika kuafikia malengo ya mkataba wa Paris wa kudhibiti wastani wa jotoridi duniani kufikia nyuzijoto 1.5.
Show more...
1 month ago
9 minutes 57 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Ripoti: Matajiri wachache wanateka nyara dunia kwa kuchangia pakubwa utoaji wa hewa ukaa
Dunia inapojiandaa kwa mkutano wa kimataifa wa Mazingira COP30 utakaofanyika Belém, Brazil, ripoti mpya imeibua mjadala mkali—si tu kuhusu uzalishaji wa hewa ukaa, bali pia kuhusu ukosefu wa usawa.
Show more...
2 months ago
9 minutes 58 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Siku ya Chakula duniani: Mapendo Banque Alimentaire yapambana na ukosefu wa usalama wa chakula
2 months ago
10 minutes 1 second

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga
Ripoti ya 2025 ya tathmini ya kidunia juu ya kupunguza hatari za majanga inakadiria kuwa gharama kamili ya kukabili majanga ni karibu dola trilioni2.3, na licha ya uwekezaji huu, bajeti za kitaifa bado ni za kiwango cha chini mno.
Show more...
2 months ago
9 minutes 50 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Vijana walioasi uhalifu na kujitosa katika kutunza mazingira ya kijiji chao
Fahamu kundi la vijana kutoka mtaa wa korogocho jijini Nairobi, walioasi uhalifu na kuamua kutunza mazingira ya jamii yao. Vijana hawa wananuia kuwa mfano kwa kizazi kijacho kufahamu kuwa hata juhudi ndogo zinaweza kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.
Show more...
3 months ago
10 minutes

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Siku ya kimataifa ya hamasisho kuhusu upotevu na uharibifu wa chakula
Wakati mamilioni ya watu wanalala njaa kila siku, chakula kizuri hutupwa mashambani, katika maduka makubwa, mikahawa - na ndiyo, hata katika nyumba zetu wenyewe. Uharibifu wa chakula sio tu kuhusu kile kilicho kwenye sahani zetu. Pia inahusu rasilimali zinazotumiwa kuzalisha chakula hicho: maji, ardhi, nishati, na raslimali watu, zote hupotea wakati chakula kinaharibika.
Show more...
3 months ago
9 minutes 59 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
ACS2: Addis Ababa: Vijana wasisitiza uwekezaji kwenye ajira za kijani
Uchumi wa kijani ni miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa kwenye mkutano wa pili wa mazingira wa bara la Afrika uliofanyika hivi majuzi jijini Addis ababa, ambapo wajumbe walijadili mikakati ya kufadhili maendeleo ya kijani barani Afrika kupitia masuluhisho yanayotegemea asili, teknolojia safi. Mjadala umeibuka kuhusu nafasi ya vijana katika mipango ya serikali za Afrika kuelekea uchumi wa kijani, kupitia ajira za kijani.
Show more...
3 months ago
10 minutes

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Oxfam: Nchi tajiri zimevunja ahadi zao za ufadhili wa hali ya hewa kwa Afrika
Ripoti mpya ya shirika la kimataifa ya Oxfam inasema kuwa nchi tajiri zimetoa tu asilimia 4 pekee ya fedha zinazohitajika Afrika Mashariki kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.
Show more...
4 months ago
9 minutes 55 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Wiki ya maji duniani na mabadiliko ya tabianchi: Changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo kame
4 months ago
9 minutes 55 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Vijana Dar es Salaam watumia teknolojia kukabili mafuriko na mabadiliko ya tabianchi
4 months ago
9 minutes 54 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mtokeo ya majadiliano ya kimataifa kuhusu mkataba wa kisheria wa kukabili taka za plastiki
Kwa mara nyingine tena, dunia ilipoteza fursa muhimu ya kuwa na mkataba huo, majadilianao yakigonga mwamba kutokana na nchi kutofautiana kwenye baadhi ya maandishi.  
Show more...
4 months ago
9 minutes 53 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
UN: Ni asilimia 35 pekee ya malengo ya maendeleo endelevu ndio yako katika njia sahihi kufikiwa
Ripoti ya malengo ya maendeleo endelevu mwaka 2025, ikiwa ni miaka kumi tangu mataifa kuanza kufanyia kazi malengo hayo. Katika ripoti hiyo, UN inasema dunia bado iko nyuma katika kuhakikisha malengo hayo 17 yanaafikiwa kikamilifu kufikia mwaka wa 2030.
Show more...
5 months ago
9 minutes 49 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mkataba wa plastiki: Mgawanyiko kuhusu jinsi ya kukabiliana na hatari ya kiafya na kiikolojia.
Mataifa mbalimbali ulimwenguni yameombwa kuchukua hatua na kutatua mzozo wa kimataifa wa plastiki, mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya kiserikali, mwanadiplomasia wa Ecuador, Luis Vayas Valdivieso akiwaomba wadau waliokusanyika Geneva, Uswizi kwa siku 10 kuunda mkataba wa kihistoria wa kuzuia uchafuzi wa plastiki.
Show more...
5 months ago
9 minutes 56 seconds

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.