Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
TV & Film
History
Technology
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts211/v4/c5/3e/cc/c53ecc68-397d-991d-b35b-5016ab775c75/mza_1256632132512185068.jpg/600x600bb.jpg
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
RFI Kiswahili
24 episodes
5 days ago

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Show more...
News
RSS
All content for Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii is the property of RFI Kiswahili and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Show more...
News
Episodes (20/24)
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio makubwa ulimwenguni katika wiki ya mwisho ya mwaka 2025
Matukio makubwa ya wiki hii ni pamoja na maadhimisho ya sikukuu ya krisimasi duniani mataifa kadhaa yakikabiliwa na shida za kiusalama, kasi ya kampeni za uchaguzi nchini Uganda, waasi wa AFC/M23 na mapigano yao mkowani Kivu kusini mashariki mwa DRC, kesi ya uhaini inayomkabili makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Macxhar kuahirishwa hadi January 06; mashambulizi ya vikosi vya Marekani dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Nigeria, na pia hali nchini Ukraine na Cambodia.
Show more...
1 week ago
20 minutes 12 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Waasi wa AFC/M23 watangaza kujiondoa mjini Uvira kwa masharti
Miongoni mwa matukio makubwa ya wiki hii ni pamoja na waasi wa AFC/M23 kutangaza kujiondoa kwenye mji wa kimkakati wa Uvira mkowani kivu kusini mashariki mwa DRC hatua ambayo imetiliwa mashaka, shirika la kimataifa la Amnesty lasema polisi nchini Tanzania walitumia nguvu kupita kiasi kudhibiti waandamanaji kipindi cha uchaguzi, wafuasi wa rais wa Tunisia, Kais Saied waandamana kuonesha ungwaji mkono huku mzozo wa kisiasa ukizidi, Umoja wa ulaya EU kuiipa Ukraine mkopo wa Yuro Bilioni 90
Show more...
2 weeks ago
20 minutes 7 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Waasi wa M23 waudhibiti mji wa Uvira DRC na maadhimisho ya uhuru nchini Kenya
Makala hii imeangazia kwa sehemu kubwa hali iliyojiri kwenye mji wa Uvira mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Kenya kutoka kwa mkoloni wake Uingereza,nacho chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania chasema watu zaidi ya elfu mbili waliuawa wakati wa machafuko ya wakati wa uchaguzi wa octoba 29, na mengine mengi
Show more...
2 weeks ago
19 minutes 44 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Rwanda na DRC zasaini mkataba wa amani Washington, chanjo ya ukimwi yaanza Afrika
Habari kuu wiki hii ni pamoja na mkataba wa amani uliosainiwa kati ya Rwanda na Drc chini ya usimamizi wa Washington, tutaangazia siasa wa Uganda na Tanzania, halkadhalika hali ya kibinadamu nchini Sudan, WHO kuonya kuhusu ongezeko la maambukizo na vifo kutokana na Malaria.
Show more...
4 weeks ago
19 minutes 58 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Rais Kagame aishutumu DRC kwa kuchelewesha amani, uchaguzi mdogo Kenya
Rais wa Rwanda Paul Kagame atuhumu DRC kwa kuchelewesha mchakato wa kumaliza vita mashariki mwa DRC, uchaguzi mdogo nchini Kenya wafuatiwa na kushambuliwa kwa mbunge wa HomaBay Town Peter Kaluma, mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea Bissau, rais wa Marekani Donald Trump asema anapanga kuzuia raia kutoka Nchi zinazoendelea kuingia nchini Marekani,tutaenda Israeli, na maeneo mengine duniani…hayo ni miongoni mwa mengi utakayosikia. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka, kusikiliza zaidi
Show more...
1 month ago
20 minutes 8 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Wanafunzi zaidi ya 200 watekwa Nigeria, tume ya kuchunguza vurugu Tanzania yaapishwa
Habari kuu wiki hii ni siasa za Tanzania zilizosababisha kuundwa kwa tume ya kuchunguza mauaji ya baada ya uchaguzi, kule DRC athari ya mafuriko, tutaangazia ripoti ya WHO kuhusu dhulma dhidi ya wanawake, kule Nigeria tutaangalia utekaji nyara wa wanafunzi zaidi ya 200 pia Mkutano wa G20 kufanyika wikendi hii Afrika Kusini Marekani ikisusia.
Show more...
1 month ago
19 minutes 58 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Rais Samia atoa msamaha kwa vijana waliokamatwa kwenye maandamano
Miongoni mwa tarifa utakazoskia katika makala haya ni pamoja na, Rais wa Tanzania Samia Suluhu, ameagiza vyombo vya sheria kuangalia uwezekano wa kuwafutia mashtaka ya uhaini mamia ya vijana waliokamatwa kufuatia vurugu za uchaguzi wa Octoba 29, lakini hayo yakijiri kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu ilihairishwa kwa muda usiojulikana.
Show more...
1 month ago
20 minutes 2 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Uchaguzi mkuu Tanzania: Waangalizi wasema haukuzingatia vigezo vya demokrasia
Katika makala yetu leo tunaangazia pakubwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania ambapo Rais Samia Suluhu aliapishwa siku ya Jumatatu kuongoza muhula wa pili, hata hivyo ni uchaguzi ambao ulikumbwa na utata huku waangalizi kutoka jumuiya ya Afrika kusini SADC na wale wa umoja wa Afrika AU wakisema haukuzingatia vigezo vya demokrasia.
Show more...
1 month ago
20 minutes 2 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Vurugu zaugubika Uchaguzi mkuu nchini Tanzania na hali nchini DRC
Uchaguzi mkuu uliofanyika katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania, na ambao uligubikwa na maandamano; mkutano wa Paris nchini Ufaransa kuhusu amani ya mashariki mwa DRC na eneo la maziwa makuu, siasa za nchini Kenya, Uganda lakini pia mauaji yaliyotekelezwa na kundi la RSF nchini Sudan, hali nchini Cameroon na Madagascar, kurejewa kwa mashambulizi nchini Ukraine, na huko Israeli dhidi ya Hamas
Show more...
2 months ago
20 minutes 6 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Rais W.Ruto amtunuku hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi, hali mashariki ya DRC
Hatua ya rais wa Kenya William Ruto kumtunuku aliyewahi kuwa waziri Mkuu na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi nchini, kukamatwa kwa makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema nchini Tanzania, John Heche, DRC na Rwanda zakubaliana juu ya mchakato wa upatikanaji wa amani chini ya upatanisho wa Marekani, uchaguzi wa urais nchini Cote D’Ivoire, na rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarcozy wiki hii alianza kukitumikia kifungo cha miaka mitano.
Show more...
2 months ago
20 minutes 3 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Kenya yaomboleza kifo cha RAILA, Jukwaa jipya la kisiasa DRC lazinduliwa
Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na wakenya kuomboleza kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Raila Amolo Odinga, kuzinduliwa kwa jukwaa jipya la kisiasa : Okoa DR Congo, kuendelea kwa kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu kule Tanzania, kuapishwa kwa kiongozi wa kijeshi wa Madagascar, na matukio mengine duniani.
Show more...
2 months ago
20 minutes 8 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Jeshi la Israeli kuondoka Gaza, rais wa DRC aitaka Rwanda kuchangia amani
Habari kuu wiki hii ni pamoja Israel kuanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye baadhi ya maeneo ya  Gaza, rais wa Ufaransa amteua tena Sebastien Lecornu kuwa waziri mkuu huku kukiwa na mvutano wa kisiasa, rais wa DRC, Félix Tshisekedi, amtaka mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, kuwaamuru waasi wa M23 kuacha vita mashariki mwa Congo, siasa za kikanda, yaliyojiri huko Morocco, mwanaharakati wa demokrasia nchini Venezuela, Maria Corina Machado, ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli ya mwaka wa 2025
Show more...
2 months ago
20 minutes 7 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Hukumu ya kifo dhidi ya rais mstaafu wa DRC, kampeni za uchaguzi nchini Uganda
Kumekuwa na hisia mseto kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya rais mstaafu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani nchini Uganda, hali ya nchini Tanzania wakati huu wananchi wakijiandaa kushiriki uchaguzi wa oktoba 29 mwaka huu, maandamano ya vijana Gen Z nchini Madagascar, na mashambulio ya mjini Manchester Uingereza.Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi 
Show more...
3 months ago
20 minutes 1 second

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mkutano wa 80 wa Umoja wa mataifa, hali ya DRC na maandalizi ya uchaguzi Uganda
Baadhi ya habari ambazo tumezipa uzito ni pamoja na mkutano wa 80 wa baraza kuu la umoja wa mataifa wiki hii ambapo viongozi wa dunia walipata nafasi ya kutoa hotuba zao, kujiuzulu kwa spika wa bunge la DRC Vital Kamerhe, na kuendelea kwa mapigano mashariki mwa nchi hiyo, kuidhinishwa kwa wagombea wa kiti cha urais nchini Uganda kuelekea uchaguzi wa mwakani, Peter Mutharika kurejea madarakani baada kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu, kura ya maoni ya Guinea, na mambo mengine mengi.
Show more...
3 months ago
20 minutes 13 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Kesi ya rais mstaafu wa DRC kurejelewa, mbio za baiskeli kung'oa nanga huko Rwanda
Baadhi ya habari ambazo tumezipa uzito ni pamoja na vurugu katika bunge la DRC na mchakato wa kumuondoa spika wa bunge hilo na maafisa wengine, mashindano ya dunia ya baiskeli kung’oa nanga siku ya Jumapili mjini Kigali, mji mkuu wa Rwanda, siasa za Uganda kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani, tumeangazia hali nchini Tanzania, Sudan kusini, uchaguzi wa Malawi, kura ya maoni kule Guinea kuhusu marekebisho ya katiba na ziara wa Marekani huko Uingereza.
Show more...
3 months ago
20 minutes 9 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Zaidi ya watu 80 wafariki katika ajali ya boti Basankusu
Karibu kwa makala ya Yaliyojiri wiki hii. Baadhi ya habari ambazo tumezipa uzito wiki hii ni makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini ashatkiwa kwa uhaini na mauaji, ajali ya boti nchini DRC.
Show more...
3 months ago
19 minutes 46 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Hukumu dhidi ya waziri Mutamba nchini DRC, athari za misaada ya kigeni watoto wakizaliwa na HIV
Wiki hii taarifa zilizokuwa gumzo kwenye vyombo vya habari ni kuhusu hukumu dhidi ya aliyekuwa waziri wa sheria nchini DRC, Constant Mutamba, nitakujuza pia kuhusu kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania, tutaangalia pia ajali ya boti nchini Nigeria iliyoua watu 30. Kimataifa, tutaangazia punde zaidi katika mzozo wa Urusi na Ukraine.
Show more...
3 months ago
20 minutes

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Kampeni za uchaguzi wa Tanzania, mapigano DRC, Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine
Kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi oktoba mwaka huu nchini Tanzania, kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame dhidi ya mzozo wa mashariki mwa DRC, mapigano makali kati ya jeshi la Congo FARDC na washirika wao wazalendo maeneo ya milima ya Fizi, hali nchini Sudan, ziara ya rais wa senegal jijini Paris ufaransa, Urusi yaendeleza mashambulio huko Kiev Ukraine licha ya shinikizo za Kimataifa na mengineyo.
Show more...
4 months ago
20 minutes 6 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mkutano wa Trump na rais wa Ukraine na wakuu wa Ulaya, hali ya mashariki mwa DRC
Ni juma ambalo limeshuhudia mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trmp na rais wa Ukraine Volodmir Zelensky akisindikizwa na viongozi wa Ulaya, michuano ya CHAN kwenye nchi tatu za Afrika Mashariki yaendelea, mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu juma hili yalishutumu jeshi la Rwanda likishirikiana na waasi wa M23 kuwaua raia wa kawaida Binza wilayani Rutshuru mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika au TICAD ulifunguliwa jijini Yokohama, Japani.
Show more...
4 months ago
20 minutes 6 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mkutano wa uswis watamatika bila mkataba wowote, mapigano Ituri DRC yaua 31
Mkutano wa Geneva washindwa kupata mkataba wa kimataifa kuhusu taka za plastiki,  takriban watu 31 wakiwemo raia 19 waliuawa katika mapigano kati ya jeshi la Kongo na wanamgambo wa CRP wa Thomas Lubanga katika eneo la Djugu mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC, michuano ya CHAN 2024 kwenye nchi za Afrika Mashariki, hali ya Sudan, Somalia na mkutano wa rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, huko Alaska.
Show more...
4 months ago
20 minutes 7 seconds

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.